WACHUNGAJI WENYE MKWANJA MREFU ZAIDI.....

Mtu wangu leo nimekuletea mwendelezo wa wachungaji wenye mkwanja (pesa) mrefu zaidi....



3. Pat Robertson

 Ndie mwanzilishi wa kituo cha Television cha Christian Broadcasting Network kinachorusha matangazo yake kutokea Virginia, kwa sasakituo hicho kinarusha matangazo yake kwenye mataifa 180. Pia aliwahi kugombea  urais wa Marekani kwenye miaka ya 80 mwishoni lakini hakufanikiwa. Anamiliki na kuendesha mashirika kadhaa ikiwepo Christian Coalition, Christian Right Organization ambalo hukusanya fedha na kuwapiga tafu wagombea wa kisiasa. Anafahamika sana kwa kipindi chake cha The 700 club.Utajiri wake unafikia dolla za kimarekani millioni 100.

 
Pat Robertson kwenye kipindi cha The 700 Club

Mjengo wa Pat Robertson

 

Pat Robertson kwenye studio a CBN Televisheni

 

3. Benny Hinn

Ni mhubiri wa kiisrael anatambulikana sana kwa mikutano yake iliyojaa miujiza - mikutano ya uamsho na uponyaji, inayofanyika kwenye viwanja vikubwa vya mpira kwenye majiji makubwa, ambayo baadae hurushwa kwenye kipindi cha televisheni kinachojulikana “This Is Your Day”. Inaaminika utajiri wake unafikia dolla za kimarekani millioni 42.

Ndege ya Benny Hinn
 
Benny Hinn kwenye moja ya mikutano yake.

Benny Hinn kwenye kipindi chake cha "This Is Your Day kinachorushwa kwenye mataifa 200


Itaendelea....

Comments

Popular Posts