HIVI NDIVYO SAMUEL ETO’O ANAVYOKULA MAISHA.......


Jina Samuel Eto’o sio geni kwa mpenda soka yeyote, hata yule ambaye anafahamu kidogo sana kuhusu soka, akiulizwa kuhusu Eto' o atasema Cameroon.Haibishaniwi kwamba ni mmoja kati ya nyota wakubwa Afrika na duniani. Inasemekana utajiri wake unafikia dolla za kimarekani millioni 85.

Safari ya mafanikio ilianzia Kadji Sport Academy huko Cameroon, baada ya kuacha masomo kutimiza ndoto yake ya kuwa mwanasoka. Alijiunga na timu ya taifa akiwa na umri wa miaka 19 tu. Amechezea vialbu vikubwa vya kimataifa kama vile Barceleona, Real Madrid, Real Mallorca zote za Uhispania. Pia amechezea vilabu vya FC Anzhi Makhachkala ya Russia, Chelsea ya England kwa uchache.

Anapenda sana magari ya kifahari kama Bugatti Veyron, a Bentley, a Lamborghini,  a Porsche, a Ferrari, Aston Martin, a Maybach Xenatec, Rolls Royce pia anamiliki Mjengo wenye thamani ya mamilioni ya dolla huko Cameroon na nje ya mijengo mingine Afrika.

Nimekuwekea picha mtu wangu zikupe moyo kwamba ndoto zako na wewe zaweza kutimia ikiwa utakusudia kufikia pale unataka kufika. Kama Eto' o ameweza kwanini wewe ushindwe.Inawezekana ukijiwekea malengo..





Comments

Popular Posts