MAKOCHA WANAOLIPWA MKWANJA MREFU ZAIDI ....
Mameneja ni watu muhimu kwenye vilabu vya soka, na wao ndio hutimuliwa au kufukuzwa kazi timu zinapokuwa hazifanyi vizuri au kufikia matarajio yaliyotarajiwa. Arsene Wenger aliwahi kusema ninamnukuu "Makocha "mameneja wa timu" ni watu muhimu sana kama sivyo kwanini hufukuzwa wakati timu wanazofundisha zinapokuwa zinafanya vibaya" Makocha/ mameneja huja na falsafa zao, na kuleta mabadiliko yenye faida kwa timu zao, na timu kubwa siku zote zimekuwa zikitafuta Makocha bora bila kujali gharama zitakazotumika.
Pep Guardiola na Jose Mourinho wote wakiwa wamesaini mikataba na vilabu vya mji wa Manchester, ndio wanaongoza kwa mbali kwa kuchukua mkwanja mrefu zaidi kuliko makocha wote duniani. Pep Guardiola anakamata paundi £15 millioni kwa mwaka kama mshahara wake kutoka kwa timu ya Manchester City kwenye mkataba wake wa miaka mitatu, wakati Jose Mourinho’ amabye pia ana mkataba wa miaka mitatu na mashetani wekundu Manchester United atakamata mpunga wa paundi £13.8 millioni kwa mwaka kama mshahara wake.
Pep Guardiola anakamata paundi £15 millioni kwa mwaka kama mshahara wake kutoka kwa timu ya Manchester City kwenye mkataba wake wa miaka mitatu |
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger alisaini mkataba mpya wa miaka 3,Mei 2014 amabao unamweka kama bosi wa Arsenak mpaka mwisho wa msimu 2016-17, kumfanya kushika nafasi ya 3 kwa ligi ya Uingereza, na wa 4 duniani. Anavuna kiasi cha paundi £8.3 millioni kwa mwaka.
Roberto Mancini ndiye meneja anayelipwa mshahara mkubwa zaidi ya wote kwenye ligi ya Italia Serie A, kiasi cha paundi £4.30 millioni kwa mwaka kwenye mkataba wake na timu ya Inter Milan wakati kocha wa Juventus Massimiliano Allegri anajipatia paundi £3.50
millioni kwa mwaka. Hata hivyo makocha hao hawamo kwenye 10 bora ya makocha wanaolipwa pesa nyingi kama mshahara.
Ifuatayo ndio orodha kamili ya makocha 7wa wanaolipwa mshahara mkubwa zaidi ya wengine duniani;
- Pep Guardiola Manchester United £15m
- Jose Mourinho Manchester City £13.8m
- Carlo Ancelotti Bayern Munich £9m
- Arsene Wenger Arsenal £8.30m
- Zinedine Zidane Real Madrid £8m
- Jurgen Klopp Liverpool £7m
- Antonio Conte Chelsea £6.5m
Comments
Post a Comment