WACHUNGAJI WENYE MKWANJA MREFU..

Inawezekana usiamini lakini ndio ukweli kwamba Watumishi wa Mungu wamekuwa wakitengeneza pesa kwa sababu ya fursa zilizopo ambazo wamekuwa wakizitumia, kama kuandika vitabu, kutengeneza filamu, kuzungumza au kuhubiri kwenye makongamano makubwa.

Wengi wao wametengeneza pesa nyingi kiasi cha kuwafanya wawe na uwezo wa kumiliki ndege binafsi, makanisa makubwa, vyombo vya habari.

Kuna baadhi yenu mtasema hawa wachungaji hawatakiwi kutenegeza pesa kiasi hicho. lakini kabla ya kuwahukumu, kumbuka hakuna mtu angependa kuishi maisha ya taabu ya kubangaiza.

Andiko hili sio kwaajili ya kumshambulia mtu ila imeandikwa kwaajili ya kuku- inspire mtu wangu wa nguvu ili uwe na ndoto kubwa. Na kama huna nia ya kutenegeneza pesa, hilo ni chaguo lako lakini hapa nakuletea wanaume na wanawake ambao wana watia moyo mengine kufanya hivyo wakati wao wenyewe wakitimiza ndoto zao.


1. Kenneth Copeland

Thamani ya vitu anavyomiliki ni millioni $760

Ndio kiongozi wa huduma ya Kenneth Copeland (Ministries). Yenye makao makuu yenye eneo la ukubwa wa ekari  1,500- mwendo wa nusu saa kutoka Fort Worth,  ambapo limejengwa kanisa. kiwanja binafsi cha ndege ya kanisa, nyumba au jengo la ku-park ndege yenye thamani ya millioni $17.5pamoja na ndege nyingine, jumba la kifahari mbele ya ziwa(Eagle Mountain Lake) huko Newark, Texas, ambako kuna uwanja wa kuchezea mpira wa tennis ( Tennis Court), gereji 6 za magari. Anakaribia kuwa billionea.



Jumba la kifahari la Mchungaji Kenneth Copeland.

 

 


2. David Oyedepo

Thamani ya vitu anavyomiliki ni millioni $150 (Nigeria)

Inasemekana kanisa (Living Faith World Outreach Ministry-Winners Chapel)lake ambalo alilianzisha mwaka 1981, ni moja kati ya makanisa makubwa Afrika.

Tayari amenunua ndege nne, na anamiliki majumba ya kifahari Marekani na Uingereza. Mchungaji Oyedepo ana miliki chuo kikuu cha (Covenant University) moja kati ya taasisi bora za elimu Nigeria na Faith Academy, Elite high School.
Mwaka 2011 Askofu David Oyedepo alinunua ndege aina ya Gulfstream V kwa dolla za kimarekani millioni 30.

Bishop Oyedepo ndani ya moja ya ndege zake nne anazomiliki.

Winners Chapel- Canaan land


Bishop Oyedepo na familia yake.

 

 Itaendelea...


Comments

Popular Posts