MATUKIO YA WIKI MICHEZONI..............
Sporting Gijon 0-5 Barcelona (Suarez, Rafinha na Neymar wakifunga wakati Barca ilipocharuka)
Luis Suarez |
Barcelona waliingia uwanjani kukipiga na Sporting Gijon bila ya nyota wao Lionel Messi lakini wakiwa katika ubora wao ule ule. Mfungaji bora wa msimu uliopitaLuis Suarez aliipa Barcelona uongozi dakika ya 29, Rafinha akafanya matokeo yawe 2-0 dakika chache baadae kuipa Barceleona umiliki wa mchezo.Luis Enrique alifanya mabadiliko kidogo mwanzo wa kipindi cha pili ili kuwapumzisha baadhi ya nyota wake kwaajili ya mechi ya mabingwa wa ulaya dhidi ya Borussia Monchegladbach.
Matokeo ya Sporting Gijon 0-5 FC Barcelona kwa ufupi:
29′ 0 – 1 Luis Suarez anafunga goli dakika ya 29 kuipa Barcelona 1-0 uongozi.
32′ 0 – 2 Rafinha anaongeza goli la pili.
81′ 0 – 3 Neymar anafunga goli la tatu.
85′ 0 – 4 Arda Turan anafanya matokeo kuwa 4-0 dakika chache baadae.
88′ 0 – 5 Neymar anakamilisha karamu ya magoli kwa kufunga goli la tano kabla ya filimbi ya mwisho.
88′ 0 – 5 Neymar anakamilisha karamu ya magoli kwa kufunga goli la tano kabla ya filimbi ya mwisho.
Comments
Post a Comment