MATUKIO YA WIKI MICHEZONI.......

Manchester United 4-1 Leicester City (Smalling, Mata, Rashford na Pogba wakifunga)

Manchester United waliwakaribisha Leicester City mwisho wa wiki iliyopita (jumamosi) katika  mchezo wa ligi kuu ya Uingereza maarufu kama PL wakiwa na presha kubwa ya kutafuta ushindi, walikuwa kwenye kiwango kizuri zaidi kipindi cha kwanza tangu kuondoka kwa Sir Alex Ferguson . 

Mourinho alimuweka benchi Rooney akianza na Rashford, Ibrahimovic na Matakwenye safu ya ushambuliaji na ikawalipa baada ya  Chris Smalling, Juan Mata, Rashford na Paul Pogba kuipatia timu yao mabao kwa nyakati tofauti tofauti.

Matukio katika mechi ya Manchester United 4-1 Leicester City kwa ufupi.
22′ 1 – 0 Chris Smalling anafunga goli kwa mpira wa kona kuipa uongozi Man United 
Smalling akiruka kufunga goli dhidi ya Leicester City.

37′ 2 – 0 Juan Mata anaipangua ngome ya Leicester na kuachia shuti kali la guu la kushoto na kufanya matokeo yawe 2-0.

40′ 3 – 0 Marcus Rashford anafunga goli baada ya mpira uliopigwa kumfikia akiwa peke yake ndani ya kumi na nane.
Rashford Akifunga goli

42′ 4 – 0 Paul Pogba anafunga goli lake la kwanza kwa Manchester United kufanya matokeo yawe 4-0 kabla ya kwenda mapumziko.
Pogba Akifunga goli lake la kwanza tangu kurudi Man United.

60′ 4 – 1 Demarai Gray anafunga goli la kufutia machozi kwa upande wa Leicester City.

Comments

Popular Posts