Mabao ya kipindi cha pili ya Gundogan na De Bruyne yaipa ushindi Manchester City 3-1 Barcelona

FC Barcelona walishuka Etihad usiku wa jumanne novemba 1, 2016 kukipiga na Manchester City kwa mara ya pili ndani ya kipindi cha wiki mbili . Iliwachukua dakika 20 Barcelona kufunga baada ya kufanya shambulizi la ghafla kumuacha Messi akitupia baada ya kuwachenga walinzi wa Man City. Hata hivyo City walirudi mchezoni baada ya kosa la kiulinzi na Sterling akamtupia pande Gundogan aliyekuwa peke yake na kuyafanya matokeo kuwa 1-1.
Manchester City 3-1 FC Barcelona kwa ufupi. 
21′ 0 – 1 Lionel Messi anaipatia Barcelona uongozi.
39′ 1 – 1 Ilkay Guendogan anaipa City goli la kwanza.
51′ 2 – 1 Kevin de Bruyne anafunga kuipa City uongozi

Comments

Popular Posts