11 WAFA BAADA YA BASI YA ABIRIA KUTEKETEA KWA MOTO...
Si chini ya watu 11 wamefariki dunia alhamis wiki hii baada
ya basi la abiria (daladala – za kinaijeria) ilipoteketea kwa moto kwenye
daraja la Otedola aneo la Berger mjini Lagos.
Taarifa zinasema kwamba wanaume wanane na wanawake watatu
walikufa papo hapo, wakati watu watatu waliokolewa kwenye ajari hiyo.
Basi iliyoteketea kwa moto. |
Inasemekana kwamba basi hilo lililokuwa linatoka Mushin
kwenda Berger lilikuwa kwenye mwendo mkali kabla ya kupinduka mara kadhaa na
kulipuka na kuteketea kwa moto.
Shuhuda wa ajari hiyo, Ojo Daramola, alisema ajari ilitokea
saa 12 jioni, na dereva alijaribu kusimamisha gari lakini hakufanikiwa.
“Nilitaka kununua
maji ghafla nikasikia mshindo sekunde chache baadae basi likalipuka na abiri
wote wakawa wamezingirwa na moto.Moto ulikuwa mkali kwa dakika kadhaa kabla ya
waokoaji hawajafika, nasikia basi lilikuwa linatokea Mushin na abiria wengi
wamekufa” Alisema.
Comments
Post a Comment