Daktari wa kimarekani mwenye asili ya Nigeria "ndio habari ya
mjini kwa sasa" kwa kiswahili cha kibongo, baada ya hivi karibuni kujenga na kuwapa nyumba 100, wajane na
watu masikini kabisa wasio na uwezo wa kupata chakula mavazi na malazi huko
Umuchukwu, kusini kwa Orumba jimbo la
Anambra huko Nigeria
Dr. Godwin Maduka ni mwanzillishi wa Taasisi na kituo cha
Afya kinachoitwa Las Vegas Pain Institute and Medical Center. Alihitimu mafunzo
ya udaktari Katika shule ya utabibu ya chuo kikuu cha Harvard tiba ya kutuliza
na kuondoa maumivu.
Kwa mujibu wa jarida la habari liitwalo “Punch newspaper”, mbali
na taaluma yake ya udaktari, amekuwa akitumikia wito wa kubadili maisha ya
jamii yake ya Umuchukwu. Kwa miaka 3, amekamilisha miradi kadhaa ya kuinua maisha
wakazi wa jamii hiyo ikiwamo:
- Ujenzi wa shule, nyumba kwa wajane, vituo vya afya, na majengo ya dini.
- Ujenzi na ukarabati wa kituo cha polisi, makazi ya polisi pamoja na ofisi ya posta
- Kugawa pikipiki 100 kwa wasio na ajira na walio kwenye dimbwi kubwa la umasikini kutoka jamii yake.
- Kuwapatia fursa ya kwenda kusoma bure wakazi wa jumuiya kwenye vyuo vikuu vya Nigeria na vya kimataifa pia
Akiongea kwa furaha, mkazi mmoja wa eneo hilo alisema, “leo
katika jamii yetu hakuna tena nyumba za majani (nyasi). Maduka ameziondoa
nyumba zote za majani kwa kujenga nyumba za kisasa za vyumba vitatu au vine”
“Nyumba zipatazo 100 tayari zimejengwa na zote kwa sasa
wamepewa wakazi wa eneo hili, hasa wajane.”
"Nimefanya hivi ili kuwasaidia watu wangu, kutokana na hali
ngumu niliyowahi kuipitia wakati nakua. Nimekuwa katika nyumba ambayo kila mara
mvua iliponyesha ilikuwa ni mateso".
"Utajiri hauna thamani kama hauwezi kuleta maisha bora ya
watu".
"Utajiri lazima utengeneze kazi kwa vijana; kujenga vituo vya
kuwapa maarifa, vibanda vya biashara kwa wanaume na wanawake, ili jamii iwe
salama” Alisema Dr. Maduka
Kupata habari zetu kwa haraka like page yetu ya facebook"Figures and Updates"
Comments
Post a Comment