MATUKIO YA WIKI MICHEZONI.....

Arsenal 3-0 Chelsea (Sanchez, Walcott na Ozil wafunga Arsenal ikirarua Chelsea ndani ya dakika 45 za kwanza)

 Arsenal walikuwa na safari ndefu baada ya kufungwa kwenye mechi yao ya ufunguzi na mahasimu wao Liverpool. Jumamosi ya jana waliikaribisha Chelsea, na kutandaza soka la hali ya juu kwa miaka ya hivi karibuni, Sanchez na Walcott wakifunga ndani ya dakika 3 na kuipa uongozi  Arsenal ndani ya dakika 15 za kwanza Mesut Ozil akafunga tena dakika ya 40 na kufanya matokeo kuwa 3-0 wa Arsernal.

Walcott akishangilia baada ya kupachika bao.

Arsenal 3-0 Chelsea kwa ufupi:
11′ 1 – 0 Alexis Sanchez anamshinda nguvu Gary Cahill na kuifungia Arsenal goli la kwanza.
14′ 2 – 0 Theo Walcott anafanya matokeo yawe 2-0 dakika moja baadae baada ya safu ya ulinzi ya Chelsea kugawanyika.
Walcott

40′ 3 – 0 Mesut Oezil anafunga goli baada ya kufanya kuzuia shambulizi la Chelsea na Kufanya shambulizi la ghafla akipeana pasi na Sanchez

Ozil akishangilia goli.

Mpaka filimbi ya mwisho inapigwa Arsenal 3 - 0 Chelsea.



Liverpool 5-1 Hull City (Lallana, Milner, Mane and Coutinho wafunga kuipa ushindi mnono Liverpool)

Adam Lallana alianza kufunga dakika ya 17 na kuipa Liverpool. El Mohamady alilimwa kadi nyekundu na   James Milner akafunga kwa penalti kufanya matokeo yawe 2 - 0. shambulizi la Sadio Mane likaipa Liverpool goli la 3 kabla ya mapumziko.

  Matokeo ya mechi kwa ufupi:
17′ 1 – 0 Adam Lallana anafunga ndani ya dakika 20 za mwamnzo kuipa Liverpool uongozi
Adam Lallana Akishangilia na wenzake baada ya kufunga goli la kwanza dhidi ya Hull City

29′ [ Red Card ] Ahmed El Mohamady anatolewa nje kwa kadi nyekundu na kufanya mambo yawe magumu kwa Liverpool.
30′ 2 – 0 James Milner anaifungia Liverpool goli kwa njia ya penalti.
36′ 3 – 0 Sadio Mane anafunga goli la tatu.
Sadio Mane akishangilia baada ya kufunga.

51′ 3 – 1 David Meyler anafunga goli lake siku hiyo.
52′ 4 – 1 Philippe Coutinho anafunga goli akiwa nje ya kumi na nane..
71′ 5 – 1 James Milner anafunga goli la tano kwa Liverpool na kukamirisha furaha ya ushindi.
James Milner akifunga moja ya magoli yake dhidi ya Hull City.



Swansea City 1-3 Manchester City (Aguero Afunga kuipa Man City ushindi wa 6 mfulurizo)



Swansea City wakiwa wamepoteza kwa Man City Katikati ya wiki kwenye michuoano ya kombe la ligi, waliwakaribisha tena Man City kwenye mechi ya ligi kuu, ambayo hata hivyo haikuwa na matokeo mazuri kwao.Sergio Aguero aliwapa bao la kuongoza Man City baada ya kupekea krossi maridadi toka kwa Sagna lakini uongozi wao ulikuwa wa mda mfupi baada ya Swansea kusawazisha goli hilo.

Swansea City 1-3 Manchester City kwa ufupi:
09′ 0 – 1 Sergio Aguero anafunga ndani ya 9 kuipa uongozi Man City.
13′ 1 – 1 Fernando Llorente anaifungia bao Swansea na kuanya matokeo yawe 1-1.
66′ 1 – 2 Sergio Aguero anafunga kuirudisha Man City kwenye uongozi.
77′ 1 – 3 Raheem Sterling anaipatia Man City goli la 3.

Comments

Popular Posts