MAGARI 7 YA KIFAHARI YANAYOMILIKIWA NA WANASOKA WA KIAFRIKA.


Wanasoka wa kiafrika wanaocheza soka ya kulipwa kwenye ligi za ulaya ni sehemu ya wanamichezo matajiri duniani, na wamekuwa wakifahamika kwa matumizi makubwa ya pesa kwa kununua magari na majumba ya kifahari. Nakuletea orodha wanasoka wanaoongoza kwa kutumia mikwanja yao kununua magari ya kifahari.



Sulley Muntari. Mchezaji huyu wa kimataifa wa Ghana anamiliki gari yenye thamani ya paundi za uingereza 135,000 aina ya Lamborghini Gallardo

Sulley Muntari na Lamborghini Gallardo

Mikel Obi Mnaijeria huyu anamiliki 2008 Bentley Continental GT yenye thamani ya paundi za uingereza 135,000 na ni sehemu tu ya moja magari ya kifahari aliyonayo.
Mikel Obi na Bentley Continental GT



Adebayor anamiliki Aston Martin DBS V12 pamoja na magari mengine ya kifahari ikiwamo Bentley, Porsche Carrera, Mercedes G Class.
Emmanuel Adebayor na Aston Martin DBS V12

Mchezaji huyu wa zamani wa Chelsea Football Club na timu ya taifa ya  Ivory Coast  anamiliki Mercedes SL65 ikiwa ni sehemu ya tu magari ya kifahari anayoyamiliki.
Mercedes SL65 ya Didier Drogba

 Obefemi Martins
Mchezaji huyu wa kimataifa wa Nigeria anamiliki Lamborghini Gallardo and a Mercedes McLaren 
Obefemi Martins na Lamborghini Gallardo


El Hadj Diouf Msenegal huyu anaendesha Mercedes McLaren SLR yenye thamani ya £400,000.


 Mercedes McLaren SLR ya El Hadj Diouf


Samuel Eto’o. Mshambuliaji huyu wa zamani wa Barcelona FC and Chelsea FC haibishaniwi ni mmoja kati ya wachezi mahiri kuwahi kutokea Afrika na duniani.Anamiliki msululu wa magari ya kifahari yenye thamani ya paundi million 4 ikiwemo Bugatti Veyron, Maybach Xenatec,  Ferrari, Aston Martin na mengineyo
Samuel Eto’o na Ferrari

Comments

Popular Posts