Daktari wa kimarekani mwenye asili ya Nigeria "ndio habari ya mjini kwa sasa" kwa kiswahili cha  kibongo, baada ya hivi karibuni kujenga na kuwapa nyumba 100, wajane na watu masikini kabisa wasio na uwezo wa kupata chakula mavazi na malazi huko Umuchukwu, kusini  kwa Orumba jimbo la Anambra huko Nigeria
 
Dr. Godwin Maduka

Dr. Godwin Maduka ni mwanzillishi wa Taasisi na kituo cha Afya kinachoitwa Las Vegas Pain Institute and Medical Center. Alihitimu mafunzo ya udaktari Katika shule ya utabibu ya chuo kikuu cha Harvard tiba ya kutuliza na kuondoa maumivu.
 
Kwa mujibu wa jarida la habari liitwalo “Punch newspaper”, mbali na taaluma yake ya udaktari, amekuwa akitumikia wito wa kubadili maisha ya jamii yake ya Umuchukwu. Kwa miaka 3, amekamilisha miradi kadhaa ya kuinua maisha wakazi wa jamii hiyo ikiwamo:



  • Ujenzi wa shule, nyumba kwa wajane, vituo vya afya, na majengo ya dini.
  • Ujenzi na ukarabati wa kituo cha polisi, makazi ya polisi pamoja na ofisi ya posta
  • Kugawa pikipiki 100 kwa wasio na ajira na walio kwenye dimbwi kubwa la umasikini kutoka jamii yake.
  •  Kuwapatia fursa ya kwenda kusoma bure wakazi wa jumuiya kwenye vyuo vikuu vya Nigeria na vya kimataifa pia
 
Akiongea kwa furaha, mkazi mmoja wa eneo hilo alisema, “leo katika jamii yetu hakuna tena nyumba za majani (nyasi). Maduka ameziondoa nyumba zote za majani kwa kujenga nyumba za kisasa za vyumba vitatu au vine”
“Nyumba zipatazo 100 tayari zimejengwa na zote kwa sasa wamepewa wakazi wa eneo hili, hasa wajane.”
  
"Nimefanya hivi ili kuwasaidia watu wangu, kutokana na hali ngumu niliyowahi kuipitia wakati nakua. Nimekuwa katika nyumba ambayo kila mara mvua iliponyesha ilikuwa ni mateso".

"Utajiri hauna thamani kama hauwezi kuleta maisha bora ya watu".

"Utajiri lazima utengeneze kazi kwa vijana; kujenga vituo vya kuwapa maarifa, vibanda vya biashara kwa wanaume na wanawake, ili jamii iwe salama” Alisema Dr. Maduka
  
Kupata habari zetu kwa haraka like page yetu ya facebook"Figures and Updates"


Comments

Popular Posts