11 WAFA BAADA YA BASI YA ABIRIA KUTEKETEA KWA MOTO...



Si chini ya watu 11 wamefariki dunia alhamis wiki hii baada ya basi la abiria (daladala – za kinaijeria) ilipoteketea kwa moto kwenye daraja la Otedola aneo la Berger mjini Lagos.
Taarifa zinasema kwamba wanaume wanane na wanawake watatu walikufa papo hapo, wakati watu watatu waliokolewa kwenye ajari hiyo.

Basi iliyoteketea kwa moto.
Inasemekana kwamba basi hilo lililokuwa linatoka Mushin kwenda Berger lilikuwa kwenye mwendo mkali kabla ya kupinduka mara kadhaa na kulipuka na kuteketea kwa moto.

 Shuhuda wa ajari hiyo, Ojo Daramola, alisema ajari ilitokea saa 12 jioni, na dereva alijaribu kusimamisha gari lakini hakufanikiwa.
 “Nilitaka kununua maji ghafla nikasikia mshindo sekunde chache baadae basi likalipuka na abiri wote wakawa wamezingirwa na moto.Moto ulikuwa mkali kwa dakika kadhaa kabla ya waokoaji hawajafika, nasikia basi lilikuwa linatokea Mushin na abiria wengi wamekufa” Alisema.

Comments

Popular Posts